WADADA waigizaji wa bongo movies, Wema Sepetu na
Kajala inadaiwa kuwa wawili hao wamemaliza tofauti zao zilizodumu kwa
muda wa miezi kadhaa.
Ambapo wawili hao inadaiwa kuwa walikuwa kama chui na paka huku sababu ya ugomvi wao kutowekwa wazi .
Kwa mujibu wa ripoti, wasanii hao waliurudisha urafiki wao uliokuwa
umetiwa doa na ‘pesa’ baada ya kukutana kwenye sherehe ya kibao kata cha
mwandishi wa magazeti ya Globalpublishers.
Baada ya sherehe hizo. Wema alipost picha inayomuonesha akiwa na Kajala,
Aunt Ezekiel na wengine na kuandika, “Mwapenda sana hawa apa,.Jana hiyo
kwa kibao kata cha imeldamtema….Ramadhan Qareem everebadi…”
Pamoja na hilo juzi kwenye akaunti ya Instagram ya @kajalacelebrity2014
ambayo bila shaka ina uhusianona muigizaji huyo, imewekwa picha ya ya
zamani ya inayomuonesha Kajala akiwa na Wema Sepetu na Prezzo na
kuandika ‘Tbt’. Na ikaimention akaunti halisi ya Kajala
Jumamosi, 5 Julai 2014
CHANZO CHA KUPATANA WEMA NA KAJALA CHABAINIKA
17:55
No comments
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)






0 comments:
Chapisha Maoni