MAMBO vipi ndugu zangu? Ni furaha yangu kwa mara nyingine tena kukutana nanyi wapendwa wasomaji wa safu yetu hii.
Tumshukuru Muumba wetu kwa kutujaalia uhai na afya njema, lakini zaidi
ya hapo tumshukuru pia kwa kutuumbia kitu mapenzi au siyo jamani? Siku
zote hatutaacha kuzungumza juu ya mapenzi kwani ni ukweli usiopingika
kwamba mapenzi ndiyo maisha yetu.
Tunafanya kazi usiku na mchana, tunahangaika huku na huko, lakini mwisho
wa siku tunafikiria jinsi gani tutapata kuboresha na kufurahia maisha
na wapenzi wetu. Tunafikiria pia ni jinsi gani tunaweza tukapata utulivu
na amani katika maisha ya kimapenzi na wapenzi
wetu, waume zetu au wake zetu katika siku zote za maisha yetu. Ndugu
zangu, Mungu ametuwekea mapenzi ili tupate raha na amani katika maisha
yetu.
Kwa maana hiyo, wale wanaoyachezea na kuyavuruga mapenzi kwa makusudi
kwa kuumiza hisia za wenzao kisha kuwasababishia vilio si watu wa
kupendeza mbele ya macho ya wale wanaojua hasa nini maana ya mapenzi.
Wanawake ni watu wa kuheshimika na kupewa furaha wanayohitaji.
Unapompata mwanamke anayekupenda na kukuheshimu, huna sababu ya kumfanya
ajute kuwa na wewe.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI!!
TUANGAZE BONGO BOFYA LIKE HAPO CHINI MDAU WETU!!
Jumamosi, 5 Julai 2014
Mfanyie mwanamke akuzidishie raha USIKU!!!
19:47
No comments
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni