Koplo wa Kitengo cha Traffiki aliyepigwa picha akiwa amevalia
sketi iliyomabana makalio amelazimika kukimbilia mahakamani kuokoa kazi yake.
Linda Okello alikimbilia Mahakamani Baada ya wakubwa wake kutaka
kumchukulia hatua ya kinidhamu wakidai alikosa nidhamu ya kazi alipovalia sketi
iliyoonesha umbo lake akiwa kazini. Dada huyo aliyezua mjadala kote duniani
kuhusu wanawake waliojaliwa makalio makubwa na kama wanabaguliwa kutokana na
maumbile yao amemshtaki Inspekta mkuu wa polisi nchini Kenya miongoni mwa tume
inayosimamia polisi nchini humo.
Linda alipigwa picha akilinda usalama katika mashindano ya mbio
za magari ya Kiambu na picha hiyo ikaenea sana katika mitandao ya kijamii
kuhusiano na urefu wake na pia makalio na umbo lake .
Sasa koplo huyo anaitaka mahakama ifutilie mbali kesi ilyoko dhidi
yake akisema,kuwa anahisi ataonewa na wakubwa wake kutokana na majaliwa yake .
Aidha koplo huyo huyo anasema kuwa japo alipewa Suruali ndefu
mbili iliasiivae tena sketi hiyo yake ,Koplo anadai kuwa bosi wake hakuwahi
kumkaripia kwa kuivalia na kuwa madai dhidi yake yanashinikizwa tu na watu
waliovutiwa na mjadala katika mitandao ya kijamii.
Taarifa ya polisi huyo kuonywa ilizua hasira kwenye mitandao ya
kijamii baadhi wakihoji ikiwa ni makosa kwa afisaa wa polisi kuvalia sketi ya
kumbana.
Source:BBC
0 comments:
Chapisha Maoni