Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii imeagiza vyombo vya dola, kukamata waganga wa jadi, wanaojitangaza kutibu
magonjwa ya Ukimwi, kisukari na shinikizo la damu.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Dk Seif Rashid alipokuwa akiwasilisha bungeni hotuba ya bajeti ya Wizara
yake kwa mwaka wa fedha 2014/15.
Aliwasihi wataalamu wa tiba asili na tiba mbadala, kuacha mara moja,
kujitangaza kuwa na uwezo wa kutoa tiba dhidi ya ugonjwa wowote ule ambao
uwezo huo haujathibitishwa kitaalamu.
“Hilo ni kosa kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha tiba asili na tiba mbadala,”
alisema.
Waziri huyo alisema yapo matangazo yanayohusu kuwa na uwezo wa kutibu Ukimwi,
kisukari na shinikizo la damu. “Kwa mujibu wa Sheria ya Tiba asili na Tiba
mbadala, matangazo hayo yaondolewe mara moja,” alisema.
Alieleza kuwa wizara itatoa mwongozo na taratibu zinazopaswa kufuatwa ili dawa
husika zithibitishwe kitaalamu.
“Napenda kuchukua fursa hii kuagiza vyombo husika vya serikali, vifuatilie
kwa karibu na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheriakwa wale watakaokwenda kinyume
na sheria,” alisema.
Waziri huyo pia alizungumzia suala la tiba za kibingwa, ili
kupunguza idadi ya wagonjwa wanaokwenda nje ya nchi kwa uchunguzi na
matibabu.
Alisema Wizara inaendelea kuanzisha huduma za tiba za kibingwa katika hospitali
za Kanda, hospitali Maalum na Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kupunguzwa
wagonjwa hao wa kwenda nje ya nchi.
Alisema huduma za upasuaji mkubwa wa moyo, zimeendelea kutolewa ambapo hadi
sasa wagonjwa 671 walipata huduma hiyo kwa mafanikio katika hospitali za
Muhimbili, Bungando na KCMC.
Aidha, wagonjwa 211 walifanyiwa upasuaji maalum katika Taasisi ya Mifupa
Muhimbili (MOI), ambapo 29 walifanyiwa upasuaji wa ubongo, 107 upasuaji
wa uti wa mgongo, 56 waliwekewa viungo bandia vya nyonga na 19 viungo bandia
vya goti.
Dk Rashid alisema katika mwaka 2014/15 Taasisi ya Mifupa Muhimbili
inatarajia kuwahudumia wagonjwa wapatao 6,900.
Aidha, itafanya upasuaji wa kuweka viungo bandia vya nyonga kwa wagonjwa 400,
kuweka viungo bandia vya goti kwa wagonjwa 150, upasuaji wa ubongo kwa wagonjwa
240, upasuaji wa uti wa mgongo na mishipa ya fahamu kwa wagonjwa 400 na
upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa 600
Alhamisi, 5 Juni 2014
WAGANGA WANAODAI KUTIBU UKIMWI SASA KUKAMATWA............
20:34
No comments
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni