Kijana mmoja mkazi wa
kijiji cha Nyambogo wilayani Rorya mkoani Mara, ambaye anadaiwa kupotea
nyumbani kwa imani za kishirikina hatimaye amepatikana huku akiwa katika hali
ya kutisha bila kujitambua na mwili wake ukiwa umejaa tope jingi, tukio ambalo
limevuta mamia ya wananchi wa kijiji hicho.
Kijana huyo Kenedy
oguko mwenye umri wa miaka 22 amekutwa nje ya nyumba yao asubuhi ya Juni 5
mwaka huu akiwa uchi wa mnyama,ambapo baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo
wamedai kuwa tangu kutoweka kwa kijana huyo siku nne zilizopita,wamekuwa
wakimtafuta bila mafanikio huku wakihusisha tukio hilo na imani za
kishirikina.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa CCM wilaya ya Rorya Bw Samwel Kiboye,ambaye ni miongoni
mwa mashuhuda wa tukio hilo amewaomba wananchi kuacha kulipiza visasi kwa
kuwasaka watu wanaotuhumiwa kwa ushirikina bali watumie vyombo vya dola
huku mwenyekiti wa kijiji hicho akilaani vikali vitendo hivyo vya ushirikina
vinavyoendelea kijijini hapo hatua ambayo amesema imesabisha wananchi sasa
kuishi kwa hofu kubwa.
Hata hivyo katika hali
ya kushangaza wazee wa jadi kijijini hapo waliagiza kila mwananchi kupita mbele
ya kijana huyo na kumpa mkono kama njia moja wapo ya kuwezesha kupata fahamu
kitendo ambacho hata hivyo hakikuzaa matunda.
0 comments:
Chapisha Maoni