Ule
ugomvi wa mashosti wawili nyota katika tasnia ya sinema Bongo, Wema Isaac
Sepetu ‘Madam’ na Kajala Masanja ‘K’, sasa umechanja mbuga hadi kufika
mjengoni, ambako inadaiwa kuwa baadhi ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, wameingilia kati ili kuumaliza.
Kwa mujibu wa chanzo
makini, baada ya mvutano wao wa muda mrefu, wabunge hao walimwita Mwenyekiti wa
Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na kumuuliza kama ni kweli
wawili hao hawaelewani.
Inadaiwa kuwa Steve
alikiri kutokuwepo kwa maelewano kati ya wawili hao ambao awali walikuwa ni
marafiki pete na kidole.
Ilisemekana kwamba
baada ya kuhakikishiwa kuwepo kwa ishu hiyo, baadhi ya wabunge hao, hasa
wapenda michezo na sanaa, walimuagiza Steve kulifanyia kazi tatizo hilo haraka,
akishindwa basi awapelekee ili wawakalishe chini.
“Walimwambia Steve
kwamba ni kitendo cha aibu kwa mastaa wakubwa kama hao kugombana, hiyo
inawapunguzia heshima kwani hiki kilikuwa ni kipindi cha kushikamana kwa umoja
ili kuisogeza mbele tasnia yao badala ya kulumbana,” kilisema chanzo hicho
kikikataa kutaja majina ya wabunge hao na kutaka aulizwe Steve.
Risasi Jumatano
liliwasiliana na Steve juu ya ukweli wa madai hayo, ambaye alikubali kuwa ni
kweli baadhi ya wabunge wamemtaka kumaliza bifu kati ya waigizaji hao maarufu
Bongo kwani nyuma yao kuna vijana wengi wanatamani kuwa kama wao.
0 comments:
Chapisha Maoni