Kuna malalamiko mengi yanatoka kwa wananume wenye
wake au wapenzi wao ambao wanajua kuendesha magari kwamba wamekuwa kiguu
na njia.
Jana nikiwa sehemu fulani, nikiwa na jamaa fulani tukawa tunapiga story
mbili tatu hivi. Huyu jamaa akaniambia kuwa mke wake tangu ajue
kuendesha gari mke wake hatulii nyumbani week end. Huwa anatafuta
visingizio mbalimbali ili kuhalalisha safari zake hizo. huwa anasingizia
anakwenda kitchen party, kupeleka watoto hospitali hata kama hawaumwi,
au kwenye bithday mbalimbali hata kama anakokwenda hakuna undugu wa
karibu au family friend. Siku za kazi wanaenda pamoja kazini na kurudi
wote mara chache kwani mwanaume ana uwezo wa kutumia gari la kazini.
Nimeamua kulitoa hapa kwa sababu hata jirani alishanilalamikia kuhusu
tabia za mke wake kuwa amekuwa kiguu na njia hasa wikiend wanapokuwa
mapumziko kwa visingizio mbalimbali ambavyo vingine vinafanana na hivyo
hapo juu.
Kwa upande wangu mimi nipo neutral, nawakarisha kama visa hivi ni vya kweli au uwongo.
Jumatano, 21 Mei 2014
Wanawake Wanaoendesha Magari Wengi ni Viruka Njia, Hawatulii Nyumbani
09:56
No comments
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni