VIGODORO, KANGAMOJA, MARUFUKU JIJINI DAR!! JIONEE HAPA
Kufuatia kuibuka kwa makundi ya kihalifu kama Panya road na Mbwa mwitu ambayo wengi wao wanahusishwa na ngoma hiyo kwenye uporaji na upigaji wa watu, Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova anasema ‘ni marufuku kwa ngoma yeyote ya asili kuchezwa nyakati za usiku’ Kamanda Kova anasema kufuatia operesheni inayoendeshwa dhidi ya vikundi hivyo vya kihalifu, mpaka sasa tayari wanawashikilia wafuasi zaidi ya mia moja ambapo pia watu wengi wamekuwa wakilalamikia vitendo viovu vinavyofanyika nyakati za usiku wakati wa ngoma hizo maarufu kama ‘vigodoro’ pamoja ‘baikoko’ na sasa jeshi la polisi limetoa onyo kali kwa watakaoendeleza hizi ngoma kuanzia sasa.
0 comments:
Chapisha Maoni