.

Jumamosi, 21 Juni 2014

Wafahamu Wasanii Wa Afrika Watakaoperform Kwenye Tuzo Za BET 2014



Tuzo za BET mwaka huu zitatolewa wikend ijayo, July 28/29 mwaka huu huko Los Angeles Marekani na kushuhudia wasanii wengi wakubwa duniani wakiperform kwenye jukwaa hilo kubwa.

Waandaaji wa tuzo hizo wameyataja majina ya wasanii watakaoperform ikiwa ni pamoja na majina ya wasanii wa Afrika. Rapper toka Ghana aliyeshinda tuzo za MTV MAMA kama msanii bora wa hip hop, Sarkodie, kundi la Mafikizolo na msanii wa kike wa Nigeria Tiwa Savage ni miongoni mwa wasanii watakaoperform.

Wasanii hao wanawania tuzo ya Best International Act pamoja na mkali kutoka Tanzania, Diamond.

All the Best Diamond Platinumz katika tuzo za BET kwa kuwa maoni ya awali yanaonesha anazungumziwa zaidi kwenye mitandao kuliko wengine.



0 comments:

Chapisha Maoni