Baada ya kupata sare dhidi ya Nigeria katika mchezo wao wa kwanza wa
kombe la dunia, timu ya taifa ya Iran leo ilikutana na Argentina.
Matokeo ya mchezo huo ni ushindi wa 1-0 kwa Argentina, shukrani kwa
goli la dakika ya tisini na moja la aliyekuwa mchezaji bora wa dunia kwa
mara nne mfululizo Lionel messi.
Iran walipoteza nafasi kadhaa za kufunga huku wakicheza vizuri dhidi ya Argentina, iliyojaa mastaa wakubwa wa soka duniani.
Kwa matokeo hayo Argentina inakata tiketi ya kuingia hatua ya mtoano ya michuano.
Jumamosi, 21 Juni 2014
Full time ya Argentina vs Iran – matokeo na alichofanya Lionel Messi
14:34
No comments
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni