Ukiona
umemtumia mpenzi wako/mchumba wako/mchepuko wako/mke wako au hata
rafiki wa kike wakati mwingine SMS ya kawaida tu kwaajili ya kumsalimia
lakini yeye akakujibu moja kati ya majibu yafuatayo, tafadhali sana
usiendelee kuchat nae maana kinachofuata hapo ni majanga tu.
KWA
MFANO: 1. Ukimtumia sms ''Mambo mpenzi wangu?'' akikujibu ''mambo
mabaya'', usimuulize kwanini mambo mabaya, ukimuuliza atakwambia kuwa
''sina hela dear''
2. Ukimtumia sms ''Maisha yanasemaje kipenzi
changu'' akikujibu ''maisha magumu hubby wangu we acha tu'' usimuulize
kwanini, ukimuuliza kwanini atakwambia ''nimefulia mwenzio kama nini
sijui''
3. Ukimtumia sms ''Mbona kimya sana mchumba wangu, umenitupa
kiasi hicho'' akikujibu ''sijakutupa wangu yaani mambo hata hayaendi''
usimuulize kwanini mambo hayaendi, ukimuuliza atakwambia kuwa ''yaani
sina kitu mpenzi wangu, simu ilikuwa haina hata hela ya kubeep''
4.
Au ukiona mwanamke anaanza kwa kukwambia nikwambie kitu? We mkatalie
kiutani utani tu, mwambie usiniambie, hata akikomaa vipi akwambie
mwambie sitaki uniambie huku unafanya kama utani lakini moyoni unakuwa
upo serious.
Ni mara chache sana mwanamke akikwambia kuwa mambo
mabaya, maisha magumu au mambo hayaendi huwa na matatizo mengine kama
kuumwa, misiba.... n.k lakini THE REST ni wapigaji mizinga tu.
Akikwambia maisha magumu mjibu ''pole wangu, mambo mengine vipi?''
Ukipewa majibu kama hayo, chagua moja, either usiendelee kuchat nae
mpaka badae kidogo au mbadilishie maada ili kukwepa huo mzinga ambao
unakuja mbele yako
Jumatatu, 8 Septemba 2014
WANAWAKE WA NAMNA HII SIO WA KUOA
04:43
No comments
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni