Wapakistani wawili, Abdul Ghan Peer Bux na Shahbaz Malk (pichani) waliokamatwa wakiwa na Watanzania wanaotuhumiwa kwa kukutwa na madawa ya kulevya wametoroka nchini.
Watuhumiwa hao walikamatwa Februari 21,
2011wakiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya shilingi bilioni
6.2, Mbezi Beach maeneo ya Jogoo jijini Dar sa Salaam.
Habari za uchunguzi ndani ya Mahakama
Kuu zinasema kuwa, Jaji Grace Mwakipesile anayesikiliza kesi hiyo
inayotarajiwa kuendelea kusikilizwa kesho Jumatano, ametoa amri ya
kukamatwa kwa watuhumiwa hao.
Kesi hiyo ambayo ilisikilizwa mahakamani
hapo Julai 4, mwaka huu ilidaiwa kuwa Wapakistani hao walikamatwa na
kikosi kazi cha kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya kisha
kudhaminiwa lakini wametoweka bila kuhudhuria mahakamani hata siku moja.
Imeelezwa kuwa, baada ya watuhumiwa hao
kudhaminiwa na wadhimini wawili, Julai 4, mwaka mahakama iliambiwa kuwa
wadhamini hao wamefariki dunia.
Hata hivyo, jaji anayesikiliza kesi hiyo
aliwaagiza ndugu waliotoa taarifa hiyo kupeleka cheti halisi cha kifo
kesho na watuhumiwa wahudhurie mahakamani hapo.
Watanzania waliokamatwa na Wapakistani
hao waliachiwa huru baada ya kulipa dhamana ya shilingi 10,000,000
ambapo wadhamini wao ni Raza Hussein Kanji ambaye alipewa stakabadhi
namba 3406367 na Nazar Mohamed Nurd alikatiwa yenye namba 3406355.
Februari 21, 2011 polisi chini ya
kamanda wao, Godfrey Nzowa waliwakamata Wapakistani hao wakiwa na
Watanzania wawili, William Chonde na Kambi Zuberi ambao wapo nje kwa
dhamana wakituhumiwa kukutwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya
shilingi bilioni 6.2.
0 comments:
Chapisha Maoni