MJADALA kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya, umeingia hatua nyingine baada ya Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Thomas Mgoli, kupigwa na kulazwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Kutokana
na hali hiyo, Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta,
amewaonya wajumbe wa bunge hilo, kuacha kuhamishia mijadala baa, kwani
ni hatari kwa maisha yao na kuwaomba Watanzania kuwa wavumilivu katika
masuala yanayohusu Katiba.
Mjumbe
huyo wa Kundi la 201 anayetoka chama cha NDC, alivamiwa na kupigwa juzi
saa mbili usiku katika duka la pombe (grocery) lenye jina la Lidya,
lililopo Area A, jirani na Shule ya Msingi Chamwino mjini hapa na
kuumizwa kwa kiasi kikubwa upande mmoja wa jicho, ambao umevimba
Akizungumza
huku akigugumia kwa maumivu hospitalini hapo, Mgoli alidai kuwa
waliompiga anawatambua kuwa ni wafuasi wa Ukawa, huku pia wakiwa wafuasi
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwani amekuwa
akizungumza nao masuala ya kisiasa katika eneo hilo mara kwa mara wakati
wakinywa pamoja.
Awatambua
“Nawafahamu
kwa sura hata na itikadi zao kwa kuwa tumekuwa tukikutana eneo hilo
kupata vinywaji. Licha ya kubishana nao masuala ya kisiasa, lakini pia
wamekuwa wakivaa magwanda ambayo ni sare ya Chadema, hivyo naijua
mielekeo yao na itikadi zao kuhusu Bunge Maalumu la Katiba, nashangaa
kwa nini wamenifanyia hivi.
“Mmoja
kati ya walionipiga anajiita Vampire (Nyonya Damu) na nimeshakutana
naye zaidi ya mara sita, tukikaa na kunywa pamoja na kujadili changamoto
ndogo ndogo sikutarajia kwamba wangefikia hatua ya kunipiga,” alisema Mgoli.
Akifafanua,
alisema alipofika katika eneo hilo juzi alikutana na wafuasi hao, ambao
walikuwa wanne na kulikuwa na mmoja ambaye ndiye alimuona kwa mara ya
kwanza siku hiyo na alijitambulisha kuwa ni mfanyakazi wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
U-CCM
“Nilienda
pale kwa nia ya kununua vinywaji, basi kwa vile huwa nawaona kwenye ile
grocery, wakaanza kunitupia maneno makali wakihoji kwa nini naunga
mkono hoja za CCM (Chama Cha Mapinduzi), hali hiyo ilinishitua kidogo.
“Niliwaambia
nimekuwa nikichangia hoja kwa maslahi ya Taifa na nikawaeleza kuwa ni
vyema hoja za kila mmoja zikaheshimiwa hata kama zinatukwaza.
“Niliposema Katiba itapatikana tu, ghafla nikashtukia nimepigwa na kitu pembeni ya jicho, kuangalia nikaona ni jiwe na watu hao wakaanza kukimbia,” alieleza Mjumbe huyo, aliyesema anaishi maeneo hayo ambako amepanga nyumba.
“Niliposema Katiba itapatikana tu, ghafla nikashtukia nimepigwa na kitu pembeni ya jicho, kuangalia nikaona ni jiwe na watu hao wakaanza kukimbia,” alieleza Mjumbe huyo, aliyesema anaishi maeneo hayo ambako amepanga nyumba.
Sitta
Kwa
upande wake, Sitta, akizungumza na Mjumbe huyo alipoenda kumjulia hali,
aliwataka Wajumbe wa Bunge Maalumu kuwa makini na maeneo wanayokaa.
Pia, alionya mijadala ya ndani ya Bunge wasiipeleke mitaani kwa vile
huko kuna watu wenye mitazamo ya aina tofauti.
“Nilikuwa
safarini ndiyo nimefika leo, nikapata hizi taarifa, nimekuja
kumuangalia Mjumbe wangu, ni tukio la kusikitisha, tunataka kujenga
jamii ya aina gani?” Alihoji na kuwataka wafuasi wa Ukawa, kutambua Bunge Maalumu la Katiba lipo kisheria.
“Ni
vyema wananchi wakiwemo wanachama wa Chadema na Ukawa, watambue kuwa
Bunge hili lipo kisheria, inashangaza kuona kuna baadhi ya watu wanataka
kulizuia Bunge Maalumu la Katiba, huku wakiwa nje ya Bunge ambalo ni la
kisheria,” alisema na kuomba kuwe na uvumilivu katika mijadala.
Alisema
haiwezekani watu wachache, wakapinga kitu kilichopo kwa mujibu wa
sheria. Alisisitiza kuwa pamoja na matukio hayo, lakini bado Watanzania
watarajie kupata Katiba nzuri.
Aliwataka
wajumbe, kutotishika na matukio hayo. Sitta alisema amesikitishwa na
tukio hilo la kutishia amani kwa Wajumbe wa Bunge Maalumu. Alisema kuwa
atahakikisha sheria inafuata mkondo wake, huku usalama ukiongezwa zaidi.
“Lakini
nawaomba Wajumbe ni vyema watumie Bunge kufanya mijadala badala ya
kuhamisha mijadala nje ya Bunge, kwani ni chanzo cha matatizo, ufike
wakati sasa mijadala hii isitoke nje ya Bunge ikiwemo maeneo ya starehe,
kwani huko inaweza kuleta madhara,’’ alisema Mwenyekiti huyo.
Polisi
Kwa
upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime, alikiri
kupigwa kwa mjumbe huyo. Alisema tayari watu watatu wanashikiliwa kwa
mahojiano kuhusu shambulio hilo, huku wengine wawili wakitafutwa.
Hata
hivyo, alisema alikuwa nje ya ofisi kwa jana, hivyo asingeweza kutaja
majina ya wanaoshikiliwa. Aliahidi kutoa taarifa kamili kwa waandishi wa
habari kuhusu tukio hilo leo.
0 comments:
Chapisha Maoni