NI laana! Baadhi ya mastaa wamenaswa laivu wakifanya vitendo
vilivyotafsiriwa kuwa vya kifuska, Ijumaa Wikienda lina mkanda kamili.
Baadhi ya mastaa wakionyeshana ufundi wa kucheza. Tukio hilo lilijiri
kwenye Ukumbi wa Letasi Lounge uliopo maeneo ya Victoria, Dar wikiendi
iliyopita ambapo kulikuwa na Kibao Kata cha mtoto wa mjini, Rose
Alphonce Nungu ‘Muna Love’.
...Ilikuwa ni full kukata mauno ndani ya Letasi Lounge. Likishuhudia
tukio hilo, Ijumaa Wikienda ambalo lilijipenyeza ndani ya nyumba,
lilifuatilia kila aina ya tukio huku likifikisha ripoti kwa mkuu wake
ambaye alikuwa ofisini akipokea matukio ya Live Dijitali.
...Burudani baada ya kukolea, hali ilikuwa hivi. Ndani ya ukumbi huo
lilishuhudia laana za aina yake ambazo zilikuwa zikiongozwa na mwenye
shughuli ambaye alikuwa akikata mauno ya ajabu kwa staili ya ‘baba na
mama’ chumbani.
Husna Maulid akionyesha ufundi.
“Duh! Yaani utafikiri watu hawajui kuwa hii ni Kwaresma, ni full laana
hebu angalia Husna Maulid, Sajent (Husna Idd) na Davina (Halima Yahya)
wakiongozwa na Muna wanavyojichetua hadi ‘makufuli’ yanaonekana,”
alisema mwanadada mmoja.
Husna Idd 'Sajent' naye akionyesha machejo yake.
Katika hatua nyingine, mwanaume tata anayejulikana kwa jina la Agrey
alivua nguo na kubaki na ‘kufuli’ kisha alipanda juu ya kiti na kuanza
kuonesha staili mbalimbali za ukataji wa mauno. “Tobaa… jamani
mwangalieni Agrey, kavua nguo anamwaga radhi…hahahaaa,” alisikika msanii
mmoja wa Kundi la Vituko Show.
...Sajent na Husna wakizidi kujiachia. Kingine kilichojiri ni pale
shindano lisilokuwa rasmi la kuzungusha nyonga lilipoibuka kati ya
watoto wa Ilala linaloongozwa na Baby Tunu na Baby Tau ambao
walishindana na watoto wa Kinondoni, Sajenti na wenzake, hali
iliyosababisha watu kushindwa kuvumilia na kuinuka vitini.
Ili kunusuru hali, mshereheshaji wa shughuli hiyo, Chumi Suleiman ‘Bi
Hindu’ alilazimika kuzima muziki kuepusha laana iliyokuwa inazidi kuvuka
mipaka.
“Jamani hata mimi nina watoto wa kiume na kike, sasa hii hali siwezi
kuivumilia, nazima muziki na shughuli ndiyo imemalizika maana wote humu
ndani tutaonekana siyo,” alisema Bi Hindu ambapo baada ya kusema tu,
aliambulia mvua ya matusi.
Read more: http://jijiletuleo.blogspot.com/2014/08/pichazhuu-ndio-ufuska-wa-mastaa-wa.html#ixzz3AHOxPvZ
Alhamisi, 14 Agosti 2014
PICHAZ..HUU NDIO UFUSKA WA MASTAA WA BONGO...JIONEE MWENYEWE HAPA...!
05:49
No comments
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni