Rais wa Manzese ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya tema mate
tuwachape Madee amefunguka na kusema kuwa anampenda na kumkubali Ney wa
mitego kutokana na ukweli kwamba mkali huyo anajua akifanyacho na
piaanajiamini katika kazi yake,Madee amefunguka na kusema hayo leo
alipokuwa akicha Live kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV katika
kipengele cha Kikaangoni Live.
Madee aliongeza kuwa licha ya Ney wa Mitego kumletea upinzani juu ya
cheo chake cha Raisi wa Manzese lakini bado ataendelea kuwa Rais wa
manzese kwa sababu dunia nzima inatambua kuwa Madee ndiyo Rais wa
Manzese na kamwe haitakuja kujirudia maana hakuna uchaguzi mwingine
uliofanyika na kamwe hautakuja fanyika hivyo yeye ndiye Rais wa manzese.
"Madee Seneda ndio rais wa manzese na dunia yote inalijua ilo,vilevile
uchaguzi mwengine haujafanyika na hautafanyika tena,so nitaendelea kuwa
raisi wa Manzese"
Ijumaa, 15 Agosti 2014
Madee:Nampenda Ney wa Mitego Ila Rais wa Manzese ni Mimi Hata Dunia Inajua Hilo
00:30
No comments
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni