Kiongozi wa kundi Kikosi cha Mizinga, Kalapina hivi karibuni alianzisha kampuni ya ulinzi iitwayo Kikosi Security na tayari walipata tenda ya kulinda stendi ya Makumbusho jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV, Kalapina alisema tofauti na makampuni mengine, Kikosi Security ina askari wazoefu katika fani ya mapigano na wengine wamepitia mafunzo ya ndondi au karate.
“Idea nzima ni kuwalinda watu na mali zao, na ilikuwa ni idea ya muda mrefu hata kwenye matamasha mengi tumekuwa tukijilinda wenyewe,” alisema Pina. “Kikosi Security tumeisajili kabisa kama kampuni. Kama unavyoona KK Security na makundi mengine. Sasa hivi ni kampuni ambayo inalinda sehemu mbalimbali lakini still bado tunatafuta sehemu mbalimbali. Tunaweza kulinda bank,” aliongeza.
“Tofauti ya security yetu na nyingine ni mafunzo na ujuzi. Security nyingine unakuta zinalinda na mapanga na marungu labda hawana mafunzo ya kupigana na kujilinda kwa maana hiyo hata linatokea balaa mwisho wa siku mali zikapotea kwa sababu hawana zile skills. Sisi tuna mafunzo mabondia wastaAfu, mabondia wakongwe, mabaUnsa, wacheza kareti kwaHiyo tupo fiti kila idara. Ndioa maana hapa stand ya makumbusho tofauti na Mwenge hakuna mateja wa kupiga piga debe, hakuna biashara ndogondogo na hakuna uhalifu wa aina yoyote. Toka tumefungua kituo hiki sasa hivi tuna mwezi mmoja na wiki ya tatu. Mimi mwenyewe nipo kwenye lindo na ninalipwa pia kwa sababu suala zima la security mimi ni professional yangu, mimi nimeshafanya security mpaka nje ya Afrika Dubai. Security imeanza kunipandisha ndege kwanza kabla ya muziki. Mwaka 2005 nilikuwa pale Emirate Dubai Umoja ya falme za Kiarabu.
0 comments:
Chapisha Maoni