Hapa ni kwenye gari safari ya kuelekea studio ndio inaanza, Mameneja Bab Tale kushoto na Salam kulia pembeni na Diamond
Hatimae mpango wa Mafikizolo wa South Africa ambao ni mastaa wa hit
single ya ‘khona’ waliochukua tuzo mbili kwenye MTV Africa music awards
2014 kufanya kolabo na Diamond umefanikiwa kwenye usiku wa June 9 2014.
Diamond pamoja na mameneja wake wawili ambao ni Salam na Bab Tale
waliongozana mpaka kwenye studio za msanii mkongwe aitwae Oskido ili
kurekodi kolabo hiyo ya Mafikizolo, kundi la Afrika kusini lililorudi
kwenye chati kupitia mikono ya Oskido.
Ndio tunawasili kwa Oskido, mtu wako wa nguvu nilikuepo kuhakikisha kila kinachotokea kinakufikia
Kama hukusikiliza Clouds FM Top 20 Jumapili ya June 8 2014, wakati wa
kufanya mazoezi ya tukio la MTV kwenye tuzo za Mama Durban South Africa
June 7 2014, Mafikizolo waliomba kurekodi wimbo na Diamond baada ya
kushawishika kufanya nae kolabo hivyo wakaahidi kushughulikia gharama
zote za kumuongezea Diamond muda wa kuendelea kukaa South Africa pamoja
na kubadili ticket ya ndege ili wakamilishe kazi yao.
Oskido
ni msanii mkubwa sana na mwenye uwezo hapa South Africa na anapendwa
sana ila pamoja na ukubwa wa jina lake, huwa hajiweki juu kabisa… ni
mpole na simple kila wakati, nakumbuka hapa yeye ndio aliomba kupiga
picha na Diamond.
Diamond
alipoingia studio alikua bado hajapewa topic ya wimbo, yani alikua
hajui wimbo unahusu nini ila dakika kadhaa baadae akaanza kushusha
mistari yake… alipoingia kuingiza voco ya kwanza Mafikizolo pamoja na
Producer wakampigia makofi na kusmile kuashiria kijana katishaa.
Bado jina la wimbo na tarehe ya kutoka havijajulikana ila kila kitu kikiwa tayari utakipata kupitia hapahapa
millardayo.com
Mafikizolo na Diamond
Upande
mwingine ambao wengi hawaujui, Diamond ni mtani na anachekesha sana,
ana aina yake ya kuhadithia kitu mpaka ukacheka… ilikua goodtimes studio
kiukweli
Hapa walikua wanacheza Theo wa Mafikizolo pamoja na Diamond.
Diamond
anaipenda sana kazi yake, yani pamoja na Mafikizolo kuondoka studio
baada ya kumaliza kurekodi… Diamond aliamua kubaki kuhakikisha roho yake
imeridhika
Ikitangaza
kutoka hapa Johannesburg South Africa leo June 10 2014 kwenye AMPLIFAYA
ya Clouds FM kuanzia saa moja usiku utasikia stori za walivyokua
studio pamoja na jinsi Mafikizolo walivyoanza kufahamu kuna mtu anaitwa
Diamond Platnumz kutoka Tanzania East Africa.
0 comments:
Chapisha Maoni