Ingawa
haijatoka rasmi taarifa za upatikanaji wa madini ya dhahabu kutoka
Samunge Loliondo ila inasemekana vijana wengi kwa sasa wameamua kwenda
kujaribu bahati yao kwenye madini hayo amabyo yanasemekana kupatikana
huko.
Taarifa kutoka kijijini mpaka sasa zinasema kuwa watu wanaongezeka
kijijini hapo kwa ajili ya kujipatia madini hayo ambayo mahali
yanakopatikana ni katika mashamba ya watu na maeneo ya kingo za mto
katika Kijiji cha Mgongo kilichopo jirani na kwa Babu.
Baada ya taarifa hizi millardayo.com
imeenda hadi makao makuu ya Wizara hiyo kwa ajili ya kujua undani wa
taarifa hizi,Badra Masoud ambaye ni Mkuu wa mawasiliano kwa umma kutoka
Wizara ya Nishati na madini ameanza kwa kusema>’taarifa hizo hata
sisi tumezikia’
‘Taarifa hizi zinafanyiwa kazi kwakweli madini yanawezekana pale yapo
ila sasa hatuwezi kuacha haya mambo yaende tu sisi tunapitia kwenye
taasisi zetu,kwa mfano pale madini watu wanasema yapo kuna Shirika letu
la GST ambalo lenyewe ndiyo linashughulika moja kwa moja na kuangalia
masuala ya madini kama kweli yapo au hayapo’
‘kwa hiyo bado tunalifanyia kazi suala hili,kingine tuna makamishna
wetu maeneo mbalimbali yakiwemo huko huko Arusha,Kilimanjaro nk. na
wenyewe kule lazima wafuate taratibu na wanachohimiza ni kuwa kama wewe
umeona kweli kuna sehemu ina madini lazima uombe leseni’.
Jumatatu, 9 Juni 2014
Majibu ya Wizara na Nishati na Madini kuhusu Dhahabu inayosemekana kuchimbwa Loliondo.
22:52
No comments
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni