.

Jumapili, 8 Juni 2014

Kauli ya kwanza ya Diamond Platnumz baada ya kushindwa kuchukua tuzo za MTV MAMA-2014






Macho na masikio ya Watanzania wengi kwa siku ya Jumamosi June 07 yote yalielekezwa Durban Afrika Kusini,  sehemu ambako zilikua zikitolewa tuzo za wateule wa MTV Afrika Music Award ‘MAMA’. 

Furaha tuliyokuwa nayo Watanzania ilikua kubwa baada ya kuona kijana wetu toka nyumbani Tanzania akiwa ni miongoni mwa vijana wanaochuana kwenye tuzo hizo tena akiwa katika  vipengele viwili,ingawa bahati haikuwa njema kwa Diamond kwani hakufanikiwa kupata tuzo  yoyote.
 
Baada ya kutangazwa washindi hao na yeye kutokuwepo Dimaond Platnumz ameandika maneno haya kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii:

"Maisha ni Hatua.. Nafkiri kwa mwaka huu ile ndio ilikuwa hatua yetu kwa MTV…Cha muhimu ni kujua wapi tulipokua mwaka jana na wapi tulipo leo… pia kujifunza na kujua ni nini cha kuongeza zaidi ili Next tym tuzidi kufanya vyema…. 


"Shukrani zangu nyingi ziende kwa Mashabiki wote,Management, Media,Family, wasanii na wadau Mbalimbali kwani kwa nguvu zao ndio zimefanya leo kunisogeza toka sehem moja kwenda nyingine…Next step #BET!!!… Asante sana #Sheriangoi kwa Suti Hii".
 
Diamond Platnumz alikuwa pia ni mmoja kati ya watumbuizaji wa ugawaji wa tuzo hizi,ambapo kwa namna alivyoingia kwenye jukwaa na Davido  ilimfurahisha kila mtu aliyekuepo ukumbini na watu waliokuwa wakiangalia nyumbani kupitia DSTV.


0 comments:

Chapisha Maoni