MKONGWE kwenye sanaa za Kibongo, Blandina Chegula ‘Johari’ amesema kufuatia vifo vya mfululizo vya wasanii, kwa kiasi kikubwa wasanii wamebadilika kitabia.
Mkongwe kwenye sanaa za Kibongo, Blandina Chegula ‘Johari’
Akipiga stori na paparazi wetu alisema, wasanii hao wamejitambua kuwa duniani watu wanapita, jambo ambalo kwa muda mrefu walikuwa wamelisahau na kuponda raha mfululizo.
“Tangu wenzetu wafariki mfululizo, wasanii wengi tumepata mshtuko na kujitambua, naona wengi wamebadilika, wamenyooka na kuanza kumrudia Mungu,” alisema Johari.
Vifo vya wasanii vilivyotokea hivi karibuni ni pamoja na cha Adam Kuambina, Sheila Haule ‘Recho’ na George Tyson.
0 comments:
Chapisha Maoni