.

Jumamosi, 7 Juni 2014

Jeshi la Polisi Linadaiwa Kuvamia Nyumbani kwa Lwakatare na Kuwakamata



Taarifa ya awali...

Katika hali ile ile ya mwendelezo wa kutumikia maelekezo na maslahi ya CCM dhidi ya wapinzani wa kisiasa wa chama hicho, Jeshi la Polisi usiku huu limevamia nyumbani kwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare na kumkamata housegirl wake.


Kama hiyo haitoshi, jeshi hilo la polisi limewakamata wafanyakazi wengine wawili (house boys) wa Lwakatare. Hadi muda mfupi uliopita vijana hao wawili, walikuwa wako Kituo cha Polisi Mbezi huku msichana wa kazi wakizunguka naye kwenye gari la patrol bila kumfikisha kituoni.


Jeshi hilo la polisi kupitia kituo hicho cha Mbezi lilikuwa linawatisha kila mtu anayekwenda hapo kituoni kuulizia sababu za vijana hao kukamatwa, lakini hatimaye mmoja wa watu walioko kituoni hapo ametonya kuwa polisi wanasema mmoja wa vijana hao kesi yake iko Arusha!


Kijana anayetaka kubambikiwa kesi huko Arusha ni mwanagenzi kabisa mjini. Hata ukimwambia aende Chalinze au Wami hawezi kupajua.


Hatimaye mbinu za CCM kupitia jeshi la polisi ya kutaka kukichafua CHADEMA au viongozi wake kwa kutumia kes za kubambikia ugaidi imerejea tena...


Tutawaletea taarifa kamili...
JF

0 comments:

Chapisha Maoni