MAMAA Majanga, Snura Mushi amekiri kutoka katika uvungu wa moyo wake
kuwa amedhibitiwa vilivyo na penzi la jamaa anayetoka naye kwa sasa
aitwaye DJ Hunter hivyo hawezi kuachika.
Mamaa Majanga, Snura Mushi akijiachia kijanja na mpenzi wake DJ Hunter.

Akipiga
stori na mwandishi wetu, Snura alifunguka kwamba tofauti na wanaume
wote aliowahi kuwa nao, DJ Hunter wanapendana kwa dhati na anaamini
ndiyo chaguo sahihi kwake. “Sijawahi kuwa na mpenzi nikamtambulisha
kwenye media bila kuwa nimempenda kwa dhati, tunapendana sana na Hunter,
hatuwezi kuachana kwa mipango ya binadamu,” alisema Snura.
0 comments:
Chapisha Maoni