Baada ya kujichora
tatuu mbalimbali mwilini mwake, kuonesha amechizika kimalovee, mwigizaji Lungi
Maulanga amechora moja yenye sura ya mpenzi wake ambaye hakutaka kumtaja.
Akipiga stori na
mwanahabari wetu, Lungi alisema kuwa ana tatuu 12 mwilini mwake ambazo
alizichorea pande za Dubai alipokuwa ameenda kutembea lakini mahaba niue ndiyo
yalimtuma achore hiyo yenye muonekano wa mchumba’ke.
“Tatuu zina maana
lakini moja nimemchora mpenzi wangu na hata nikikutana na mwanaume yeyote
anajifanya ananihitaji ajue kabisa ninaye nimpendae zaidi kwani tatuu hii
siwezi kuifuta,” alisema Lungi ambaye amechafuka tatuu katika maeneo mbalimbali
ikiwemo kwenye titi, paja na kiuno.
0 comments:
Chapisha Maoni