Bunge la bajeti linaendelea Dodoma Tanzania ambapo leo May 27 2014 kwenye kipindi cha maswali na majibu asubuhi, moja ya majibu yaliyotolewa ni kuhusu uwepo wa mbio za mwenge na gharama zake.
Naibu waziri wa habari
vijana utamaduni na michezo Juma Nkamia amesema serikali kuu hutenga kiasi cha
fedha kulingana na mahitaji na gharama halisi ya wakati husika ambapo mwaka
2012 jumla ya shilingi milioni mia sita hamsini (650) zilitengwa kwa ajili ya
kuadhimisha uzinduzi na kilele cha mbio za mwenge wa uhuru na kati ya hizo
milioni 450 zilitumiwa na Wizara na milioni 200 zilitumiwa na mkoa uliokua
mwenyeji wa sherehe za kilele
Kuhusu kiasi cha fedha
kinachotumiwa na wilaya, ni kwamba zinatofautiana kulingana na michango ya
Wananchi katika wilaya husika kwani michango hiyo ni kwa ajili ya miradi ya
maendeleo ambayo huzinduliwa wakati ya mbio za mwenge, kwa ujumla mwaka 2012
Wananchi walichangia zaidi ya Bilioni 11 na milioni 500.
Halmashauri za wilaya
na manispaa zilichangia shilingi Bilioni 45, Wahisani na watu binafsi
walichangia zaidi ya shilingi milioni 52 ambapo faida zinazopatikana kutokana
na Mwenge wa Uhuru nchini ni pamoja na kuendelea kutunza historia na falsafa ya
ukombozi wa taifa letu, kuhamasisha Wananchi kuhusu umuhimu wa kuendelea kuenzi
amani, mshikamano, upendo na zaidi kupambana na ubaguzi wa dini, rangi au
ukabila
Mbio za mwenge wa
uhuru hutumika kuhimiza miradi mbalimbali kwa njia ya kuweka mawe ya msingi au
kuzindua miradi iliyowekewa jiwe la msingi mwaka uliopita na pia kuhamasisha
moyo wa Wazalendo na kujitolea kwa vijana hasa kuonyesha umuhimu na nafasi yao
katika kudumisha nchi yao, kulinda uhuru na kuleta maendeleo ya nchi yao
0 comments:
Chapisha Maoni