Watu wa karibu wa
Mtuhumiwa huyu walijitokeza Mahakamani ili kuangalia kama ndugu yao aitwae
Simon Ngozi (21) ataweza kupata dhamana kwenye kesi inayomkabili ya kubaka
mtoto wa miaka tisa.
Jamaa alikua
amepelekwa Mahakamani Makadara Nairobi nchini Kenya
lakini ghafla akamshangaza kila mtu baada ya kutaka kumbaka Mwanamke aliyekua
karibu yake baada ya kuanza kumshikashika.
Mshukiwa huyu alikuwa
kortini kujibu tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka tisa April 2014 ambapo wakati
anataka kumbaka Mwanamke huyu Mahakamani tena kwenye eneo la wazi, alimpiga
mtama kwanza Mwanamke huyo lakini kwenye purukushani zake hakufanikiwa manake
Polisi walimuwahi.
Shughuli za Mahakama
zilisimama kwa muda baada ya tukio hilo kutokea ambapo baada ya hapo Mwanamke
aliyetaka kubakwa alisema, "Nilikua nimeketi karibu naye na mara ya
kwanza alilishika begi langu nikalisogeza mbali nikidhani ni mwizi lakini bila
aibu akanishikashika tumboni kabla ya kunisukuma nikaanguka sakafuni"
Baada ya hapo dada wa
mtuhumiwa alimuomba mwanamke huyo kumsamehe ndugu yake akisema yuko katika hali
hiyo baada ya mchumba wake kumtoroka kwa sababu ya kesi ya ubakaji.
0 comments:
Chapisha Maoni