Katika hali isiyokuwa
ya kawaida na kushtua wasanii Jakob Steven Jb na Steve Magele Nyerere
wamepigana ngumi kavukavu karibu na eneo la msiba wa marehemu Adam
Kuambiana huko Bunju huku kisa kikiwa kugeukana kwenye dili la matangazo.
Kwa mujibu wa tovuti
ya maskanibongotz, msanii steve nyerere ndiye aliyeanza kumchokoza msanii Jb
kwa kumchana baada ya kumgeuka kwenye mchongo wa matangazo ya kampuni moja ya
simu iliyopo maeneo ya Moroco Jijini Dar.
Habari zaidi zilisema
wakati wasanii hao wakiwa baa wanakula kilaji siku moja kabla ya mazishi ya
msanii mwenzao, Steve alimvamia Jb na kuanza kumchana na kumueleza jinsi
alivyokuwa na roho mbaya kwa kumgeuka kwenye mchongo wa mtangazo ya simu pale
Moroco ..
Majibizano hayo
yalidumu kwa muda mrefu huku Jb akiwa kimya kwani stevu alionekana
kuumizwa na jambo hilo kwani inadaiwa zile picha za Jb kwenye mabango ya mtandao
huo wa simu mchongo alipewa steve lakini baadae Jb alimgeuka na kwenda
kupiga mchongo kimaya kimya na kumuacha Steve akishangaa.
Steve aliendelea
kumsasambua Jb mbele ya watu, hali iliyomfanya Jb kunyanyuka na kuanza
kumfokea huku akimtishia kumfinyangafinya na ufupi wake ndipo steve nyerere
aliyekuwa ameshika chupa ya kilaji aliruka kichwa kimoja kilichompiga Jb
kifuani na kupepesuka.
0 comments:
Chapisha Maoni