Imezoeleka kuwa shindano la Big Brother Africa huwa linaanza mwezi May lakini la mwaka huu 2014 kutokana na kombe la dunia, litaanza September 7 ikiwa ni season 9 ambapo awamu hii idadi ya nchi zinazoshiriki ni ileile ya nchi 14 ila kuna nchi moja imeondolewa.
Angola wameondolewa na
sasa Rwanda wameingizwa kwa mara ya kwanza huku nchi nyingine zitakazoshiriki
zikitajwa kuwa ni Botswana, Ethiopia, Ghana, Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria,
Sierra Leone, Rwanda, South Africa, Tanzania, Uganda, Zambia and Zimbabwe.
Washiriki wote ni
kuanzia umri wa miaka 21 ambao ni lazima wawe ni Wananchi wa hizo nchi
zenyewe na wawe na hati za kusaifiria kutoka nchi hizo.
Tarehe za kuwasaka
washiriki wa mwaka huu zitatangazwa mwezi wa sita .
0 comments:
Chapisha Maoni