**********
Hofu ya ushirikina imetikisa Mkoa wa Arusha kufuatia tukio la hivi karibuni ambapo mwanafunzi wa Chuo cha Kompyuta jiji hapa, Witness Obed (21) aliyefariki dunia Aprili 12, mwaka huu na kuzikwa kwenye makaburi ya nyumbani kwao Kijiji cha Nanja, Kata ya Moshono wilayani Arumeru, Arusha kuibuka akiwa hai.
Binti huyo aliibuka
kwao hivi karibuni akiwa mpole na kuwafanya baadhi ya watu, wakiwemo wazazi
wake kutimua mbio kwa hofu.
Watu kutoka maeneo
mbalimbali jijini hapa wamekuwa wakimiminika nyumbani kwa wazazi wa binti
huyo kwa lengo la kumshuhudia kwa vile ndugu walishaamini kuwa, mpendwa wao
huyo alishakufa na alizikwa.
Umati wa watu ukiwa
katika hali ya mshangao kutokana na tukio hilo.
UWAZI LATIA TIMU
NYUMBANI
Baada ya kusikia
taarifa hizo, Uwazi lilifunga safari mpaka eneo la tukio na kumshuhudia binti
huyo kisha likaenda kwenye kaburi alilozikwa.
Kwenye kaburi hilo,
msalaba wenye kuonesha siku yake ya kuzaliwa (1992) na kufa (12, Aprili, 2014)
ulikuwa bado umesimama imara huku kaburi lenyewe likionesha dalili ya kutitia
kidogo.
BABA MZAZI ASIMULIA
Akisimulia mkasa huo
kwa mshangao mkubwa, baba mzazi wa binti huyo, Obed Leiyo alisema:
“Ilikuwa Aprili
mwanzoni, binti yangu alitoweka nyumbani baada ya kurudi kutoka chuoni
majira ya saa 2 usiku akiwa amechelewa.
Hili ni kaburi alipozikwa
Witness Obeid Leiyo.
"Mimi kama mzazi
nilimfokea kwa kuchelewa kwake kurudi nyumbani.
“Yeye kwa hasira zake
alizunguka nyumba akaondoka muda huohuo na hakurudi kabisa hapa nyumbani.
“Siku iliyofuata
tulianza kumtafuta maeneo mbalimbali bila mafanikio, tukatoa matangazo kwenye
vyombo vya habari lakini binti yangu hakuonekana.”
TAARIFA ZAFIKA, KAFA
Mzazi huyo aliendelea
kusema: “Siku moja tulipata taarifa kwamba kuna mwili wa msichana
umeonekana katika Kijiji cha Bwawani hapahapa Arumeru.
“Mimi pamoja na ndugu
wengine tuliamua kwenda katika kile kijiji. Tulipofika tuliambiwa ni kweli
mwili wa msichana uliokotwa lakini wananchi wakauzika.”
WAFUKUA KABURI
Baba huyo anaendelea: “Niliamua
kwenda Kituo cha Polisi cha Usa River ambako niliomba kibali kwa ajili ya
kufukua kaburi na kuutoa mwili ili kuutambua kama ni binti yangu au la!
“Nilipewa kibali,
tukafukua kaburi na kutoa mwili. Nilimtambua kuwa ni binti yangu kutokana na
alama mbalimbali alizokuwa nazo, ikiwemo rangi kwenye kucha na sehemu ya
kushoto ya uso ilikuwa nyeusi kwa sababu aliwahi kupooza."
Witness akiwa na baba
yake mzazi, Bw. Obeid Leiyo Mara baada ya kurudi nyumbani akiwa hai.
MWILI WASAFIRISHWA,
WAZIKWA
Baba huyo wa Witness
alizidi kueleza kuwa waliusafirisha mwili huo hadi nyumbani kwake Moshono na
kuandaa taratibu za mazishi ambapo Aprili 23, mwaka huu mwili ulizikwa.
AIBUKA GHAFLA
Hata hivyo, Obed
anasema alishangaa siku ya tukio kumwona binti yake huyo akiibuka nyumbani hapo
akiwa hai jambo ambalo lilimshangaza na kumfanya akimbie kwanza na baadaye
kufanya mawasiliano naye.
BINTI ASIMULIA
Akizungumza na Uwazi,
binti huyo alikiri kutoweka nyumbani kwao Aprili 15, mwaka huu na kwenda
kusikojulikana.
Alisema hakujua
kilichoendelea baada ya kuondoka nyumbani lakini baadaye alibaini kuwa alikuwa
katika Kijiji cha Olkokola wilayani Arumeru na alikwenda kwenye nyumba ya
mwanamke mmoja asiyefahamiana naye akamuomba maji ya kunywa.
“Nilifika kwenye
nyumba moja nikamkuta mama mmoja, nikamwomba maji ya kunywa akaenda kuniletea.
Nilikunywa huku amenisimamia, lakini maji yalikuwa machungu sana,
nikamrudishia, akanilazimisha ninywe kwa kunisukumia kikombe kinywani.
Nilipomaliza nilipoteza fahamu.
“Baadaye nilizinduka,
nikaendelea kuishi palepale nyumbani kwa yule mama lakini sifahamu nilikuwa
nafanya nini.
“Juzi ndiyo
nikashangaa kujikuta nimerudi nyumbani, mimi sijui nini kilikuwa kikiendelea,” alisema binti huyo.
MAJIRANI NAO
Majirani kadhaa
waliokuwepo nyumbani kwa Obed walilielezea tukio hilo kwamba ni la ushirikina
huku wakisema ni jambo la kuogofya ambalo halikuwahi kutokea kijijini hapo
kabla.
Wengine walisema kuwa
binti huyo alifufuka na wengine walisema alichukuliwa msukule.
“Hili si suala la
kawaida lazima kuna ushirikina kwani huyu binti tulishamzika na wazazi wake walimtambua
kabisa kuwa ni yeye baada ya kuambiwa alikutwa amekufa, sasa hebu fikiria tangu
tumezika mbona hakuna mtu aliyekuja na kusema na yeye alipotelewa na binti yake
halafu cha ajabu hilo kaburi mbona limebonyea? Atakuwa amefufuka," alisema mkazi mmoja
aliyejitambulisha kwa jina la Amina Liwa.
Mkuu wa Polisi wa
Kituo cha Usa River, Benedict Mpujila amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kusema uchunguzi unafanyika.
KUMBUKUMBU
Mapema mwaka jana
tukio la kishirikina liliibuka katika wilayani Arumeru eneo la Kwa Mrefu ambapo
mtu mmoja alidaiwa kudondoka na ungo, muda mfupi baadaye alitoweka na kwenye
ungo kubaki mayai na kuku mweupe.
Chanzo:
Gazeti la Uwazi/GPL









0 comments:
Chapisha Maoni