
Msanii wa muziki wa Bongo Flava kutoka Tanzania Diamond Platnumz, amekuwa akiwakimbiza katika upigiwaji wa kura kuwania tuzo za Muziki wa Televisheni ya Watu Weusi Marekani (Black Entertainment Television-BET) katika kipengele cha Best International Act: Africa. Tuzo hizo zitatolewa jijini Los Angeles, Marekani Juni 29, 2014.
Mpaka jioni hii, Mei 19, Diamond anaongoza kwa asilimia 75.79 akiwa amewaacha wengine nyuma sana.
0 comments:
Chapisha Maoni