.

Jumanne, 17 Juni 2014

UNAAMBIWA HUYU NDIYE MSANII WA BONGO MUVI MWENYE SURA YA UPOLE ALIYEMSHUSHIA PRODUCER KIPONDO HOTELINI

Stori: Emelder Tarimo
WHY? Mwigizaji mwenye sura ya upole, Riyama Ally amezua utata akidaiwa kumshushia varangati rafiki yake kipenzi, Prodyuza Emmanuel Sewando ‘Manecky’ baada ya kumkuta akiponda raha na mwanamke hotelini.


Mwigizaji wa Bongo Muvi, Riyama Ally. Ilielezwa kuwa tukio hilo lilitokea juzikati kwenye hoteli moja iliyopo Kijitonyama, Dar ambapo mastaa wengi huenda kuogelea lakini Riyama hakufurahishwa na kitendo hicho cha Manecky kuwa na mwanamke, akalianzisha.

Prodyuza Emmanuel Sewando ‘Manecky’. Alipotafutwa Riyama alisema: “No Comment.” Lakini kwa upande wake Manecky, alisema:
“Wananipakazia jamani sikuwa mimi hiyo sehemu bali kuna mtu wamenifananisha naye.”
Wawili hao wamekuwa wakitajwa kuwa wanatoka lakini wenyewe wamekuwa wakikanusha.

0 comments:

Chapisha Maoni