
Staa wa bongofleva Shetta ameongea exclusive na DStv.com baada ya kupatikana hiyo nafasi nikitaka kujua uwezekano wa kolabo yake na Diamond kwa mara ya tatu.
Kwa sasa Shetta ana single ya pili aliyofanya na Diamond Platnumz Kerewa ambapo amethibitisha kwamba kuna ya tatu inakuja.
Shetta anasema: "Unajua watu hawajui lakini Diamond ni mshkaji wangu sana, huwa tofauti na kazi tunakua pamoja sana mitaani, so nilirekodi wimbo mpya Diamond alivyokuja studio akasema na yeye anataka kuingiza voco japo sikuwa nimemshirikisha."
"Humo ndani Diamond amesema atachana yani tofauti na watu walivyozoea kumuona au kumsikia akiimba, siwezi kuzuia kuendelea kufanya kazi na Diamond... ni mshkaji wangu sana."
Diamond na Shetta wako mbioni kwenda kufanya video ya Kerewa nchini South Africa hivyo kaa karibu na DStv.com ili kupata kitakachoendelea. Video ikitokea hivi tarajia kupata exclusive papa hapa!
0 comments:
Chapisha Maoni