Msanii wa Hip Hop kutoka Morogoro, Resilience ametoa sababu ya nyimbo nyingi za bongo zinazofanyiwa remix kutofanya vizuri hapa nyumbani.
Resilience aliitolea mfano remix ya ‘Number One’ ya Diamond na Davido kwa kudai kuwa msanii huyo alijua timing pamoja na thamani ya msanii aliyefanya naye.
“Diamond remix yake ilifanya vizuri kwasababu kwanza nyimbo ilikuwa hit, pili alijua kucheza na timing kitu ambacho ni cha umuhimu sana,” Resilience aliambia Bongo5. “Na tatu jinsi alivyopandisha thamani ya wimbo huo kwa kufanya kolabo na msanii mkubwa Africa kama Davido. Sasa kwanini isifanye vizuri? Kwahiyo timing, yaani muda wa kutoa hiyo remix. Kwasababu hauwezi kutoka remix kabla haijatoka original version. Unakuta original version imekufa wewe unadhani kufanya remix ndo utairudisha? Umefanya nyimbo ya masikitiko, nyimbo ya masikitiko unaifanyiaje remix, unataka usikitike nini zaidi? Remix nyingi zinakuwa ni nyimbo za party au nyimbo za umimi. Yaani zile nyimbo za kama kutuNishiana na kuoneshana nani zaidi. Kwahiyo tatizo kubwa wasanii wengi wanakosa kujua mambo kama hayo,” alisema Resilience. - See more at: http://winternews1.blogspot.com/2014/10/stamina-aeleza-kwanini-remix-ya-number.html#sthash.5e9Rea4y.dpuf
Jumatatu, 6 Oktoba 2014
Stamina aeleza kwanini remix ya ‘Number 1′ ilihit kuliko remix za nyimbo zingine za Bongo
19:58
No comments
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni