Ile hatua ya U boifriend na U girlfriend ikiwa
imepita na kuingia katika hatua ya uchumba wa mahaba kedekede, dada yetu
Diva alijikuta anamwaga chozi baada ya watu mbalimbali kumtupia maneno
kwamba amempendea King Crazy Gk umaarufu wake ili abaki kupata KIKI
Mjini.
Diva alijikuta anatoa maneno makali ya hasira na kuangua kilio na kudai
kuwa hajampendea Gk umaarufu wake sababu yeye ni Diva ni maarufu pia
hapa Tanzania, hakuishia hapo alizidi kudai ya kuwa amechoshwa na watu
wengi kusema ana mahusiano na Gk ambae hana Pesa na ameachana na
mwanaume ambae anapesa na cheo kikubwa Tanzania.
Diva:Nimechoshwa kuulizwa maswali ya Prezzo au mwanasiasa sababu huko
siko tena na sina mahusiano nao zaidi ya urafiki wa kawaida wa kuongea
nao kama watanzania wenzangu na pili amedai kuwa hana hisia zozote za
kimapenzi na watu hao sababu yeye yuko na Mpenzi wake na anafurahia
mapenzi hayo na mume wake ambae ni Mungu wa Muziki Tanzania.
Diva Binti mwenye mvuto na umbo la kuvutia na mvuto wa sura ya babyface
na macho ya duara alidai kuwa King Crazy Gk ni Mtu mwenye kipato kizuri
tu ila sio mtu wa kujionyesha au kuishi maisha ya kujionyesha na ni mtu
mtaratibu anaeishi maisha yake alioridhika nayo na anatumia pesa zake
kulipia elimu na kufanya mambo yake na biashara zake binafsi tofauti na
watu wanavyomfikiria. Diva la Diva alisema kuwa Hakumpendea Gk Pesa au
Umaarufu wake amempenda yeye kama yeye na anachukia baadhi ya watu
kumuingilia kimawazo maisha yake ya mapenzi ambayo mashabiki wengi
wameonekana kuvutiwa nayo kupitia mtandao wa instagram
Ijumaa, 22 Agosti 2014
SOMA HAPA KIPYA ALICHOKISEMA DIVA KUHUSU PENZI LAKE KWA CRAZY GK
05:22
No comments
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni