.

Ijumaa, 1 Agosti 2014

NDOA YA LUCY KOMBA NA MZUNGU WAKE INANING'INIA SHIMONI..! SOMA ZAIDI HAPA Bagikan



Staa wa filamu Bongo, Lucy Francis Komba 
akiwa na mchumba wake.HUKU akiwa kwenye
vikao vya maandalizi ya harusi na Mzungu, staa
wa filamu Bongo, Lucy Francis Komba
(pichani na mchumba wake), amejikuta katika
wakati mgumu baada ya habari kudai kwamba,
mchumba wake huyo amemwambia ili ndoa
ifungwe lazima aoneshe cheti cha kipimo cha
Ukimwi kwanza.
Chanzo chetu cha habari kikizungumza na Amani
juzi, kilisema kwa
sasa Lucy anahaha kutafuta cheti feki cha 
kipimo hicho kwa kwenda hospitali mbalimbali ili 
anunue kwa gharama yoyote lakini imeshindikana.

“Ukweli Lucy anahaha kutafuta cheti cha Ukimwi, mchumba anasubiri akione vinginevyo hawatafunga 
ndoa,” kilisema chanzo.
Ilidaiwa kuwa, mpaka sasa Lucy ameshafika 
kwenye hospitali tatu kubwa mbili, TMJ na 
Marie Stopes ili kufanya maarifa lakini 
imeshindikana.

Baada ya kupata habari hizo paparazi wetu 
alimtafuta 
Lucy ambapo alikuwa na haya ya kusema:

“Si kweli! Hao wanaosema hivyo ni wanafiki, 
sijui wanataka nini maana kila siku wanazusha 
mambo ya ajabu. Kwanza mimi huwa 
sitibiwagi kwenye hospitali hizo ulizozisema, 
natibiwa Regency.

 Lucy Francis Komba. “Kuhusu kupima Ukimwi, 
mimi na mchumba wangu tulishapima hukohuko
kwao Ulaya (Denmark) ndiyo maana tukaanza 
taratibu za ndoa.

“Namshangaa sana huyo aliyesema hayo hata
kama ni mtu wangu wa karibu, mimi huwa
simwelezi
mtu mambo yangu binafsi kwa sababu duniani 
hakuna rafiki wa kweli, rafiki anakuchekea 
machoni
lakini wote ni wabaya,” alisema Lucy.

Amani lilifika kwenye hospitali hizo lakini
kukakosekana ushirikiano kwa madai 
kwamba, 
hakuna utaratibu wa kumtaja jina mgonjwa
kama alikwenda kutibiwa.

0 comments:

Chapisha Maoni