Mwanamitindo raia wa Sudan aishie Marekani, Ataui Deng aliyepotea kwa
muda wa wiki mbili huku akitafutwa na polisi amekutwa akiwa hai katika
hospitali moja nchini humo.
Marafiki wa mwanamitindo huyo walitoa taarifa polisi na kuanzisha
kampeni maalum ya kumtafuta baada ya kushindwa kumpata kwa kipindi
kirefu, kampeni ambayo iliungwa mkono na watu maarufu akiwemo Rihanna.
“Kama mtu yoyote ameshapata taarifa kuhusu alipo huyo binti mdogo,
tafadhali wapigie kitengo cha polisi cha Newyork (NYPD) au tuma barua
pepe findataui@gmail.com.” Ilieleza tweet ya Rihanna.
Boyfriend wake, Grand Monohon alisema kuwa mara ya mwisho alimwambia
kuwa anaaka kwenda mbali lakini aliacha simu na kila kitu chake nyumbani
kwao.
Hakuna taarifa rasmi zilizotolewa kuhusu hali ya Autui hadi sasa.
Kwa mujibu wa polisi, Ataui aliyeingia nchini Marekani kama mkimbizi
akitokea kwao Sudan, alionekana kwa mara ya mwisho August, 6 majira ya
saa tano usiku.
Jumatano, 20 Agosti 2014
Mwanamitindo Msudan 'Ataui Deng' aliyepotea wiki mbili Marekani akutwa hospitalini
07:03
No comments
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni