.

Jumatano, 6 Agosti 2014

MTOTO WA OBAMA AMPIGA MTU TEKE

Comment za Facebook zaid ya 8300 na Tweet zaidi ya 8000 Marekani peke yake zilijadili ajenda moja ya inayomhusu mtoto wa Rais Obama anaefahamika kwa jina la Malia.





Achilia mbali "COMMENTS" za Ulimwengu mzima pamoja na "LIKES" za mitandao mingine ya kijamii ambazo ziliacha kujadili mambo mengine na kujadili waandishi pamoja na tukio alilofanya mtoto huyo wa kwanza wa Rais wa Marekani.


Watoa comment hao hawakujadili kitendo cha mtoto Malia Obama (16) kuibukia katika tamasha la muziki lijulikanalo kama Lollapalooza ambalo lilifanyika Chicago kwa siku tatu huku binti huyo akiwa amevalia mavazi mepesi yanayoendana na sehem husika akiwa na marafiki zake watatu.


Pia hawakujadili kitendo cha Ikulu ya nchi hiyo kutokutoa taarifa kuwa binti huyo atahudhuria tamasha hilo lilioaza July 31, lililofanyika siku tatu mfululizo.


Hata hivyo ubishani mkubwa ulitokana na kitendo cha mitandao mingi ya habari ikiwemo Yahoo kuandika tukio la mtoto wa Obama kumpiga teke kwa bahati mbaya binti mmoja wa Uturuki Bridget Truskey katika harakat za kushangilia, ambapo binti huyo katika ukurasa wake wa Twitter alieleza kufurahishwa na kitendo cha kupigwa teke na mtoto wa Obama.


Katika comment za Facebook na Twitter, wengi waliwalaumu waandishi wa habari kuwa wamekosa mambo ya kuandika huku wengine wakisema waandishi wa habari hawana jipya na taaluma hiyo inaelekea kufa.



Picha ya Selfie iliyopigwa familia ya Obama katika tamasha la Jay Z & Beyonce


Hivi karibuni familia ya Obama ilihudhuria tamasha la Jay na Beyonce ambapo mrembo mmoja alifanikiwa kupiga picha ya SELFIE na kuiweka instergram ambapo watumiaji wengi walishanga kwakua si kawaida, lakini pia tamasha la Lollapalooza, mtumiaji mmoja waTwitter (Sarah) alifanikiwa kumpiga picha Malia akiwa mdomo kwa furaha wazi katika tamasha la Lollapalooza na kuipost.

0 comments:

Chapisha Maoni