NYOTA wa muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ ambaye hivi
karibuni ndoa yake iliripotiwa kuwa katika sintofahamu na kuvunjika,
anadaiwa kuhamia katika hoteli moja yenye hadhi ya nyota tatu iliyopo
Oysterbay jijini Dar.
Nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Jide amekuwa akionekana akiingia na kutoka
kwenye hoteli hiyo huku nyumba yake iliyopo Kimara-Temboni, Dar ikiwa
haina mkazi wa kudumu.
Wiki iliyopita, kulienea taarifa katika mitandao ya kijamii ikieleza
kuvunjika kwa ndoa ya Jide na mume wake, Gardner Gabriel Fikirini
Habash. Wawili hao walifunga ndoa mwaka 2005.
Taarifa zikadai kwamba Gardner naye aliondoka nyumbani hapo na kwamba hivi sasa anaishi kwa mmoja wa ndugu zake.
Hata hivyo, gazeti dada ya hili, Ijumaa toleo la Ijumaa iliyopita
lilizungumza na Gardner ambaye pia ni meneja wa msanii huyo, lakini
alikanusha vikali uvumi huo akisema si kweli.
Kufuatia madai hayo, mapaparazi wetu walikwenda hadi nyumbani kwa nyota
hao ambapo hakukuonekana dalili za kuwepo kwa mtu ndani.
Judith Wambura ‘Jide’ akipozi.
Baadhi ya majirani walioulizwa, walisema mara ya mwisho walimuona
Gardner miezi miwili iliyopita akiwa na basi la Bendi ya Machozi lakini
hawaelewi kwa sasa wanaishi wapi na wakoje katika ndoa yao!
Juzi, mapaparazi wetu walipiga kambi hotelini hapo ambapo mfanyakazi
mmoja wa hoteli hiyo alisema, Jide anaishi hotelini hapo na kwamba
kutokana na kuwa mteja wa muda mrefu, hata kadi ya kufungulia mlango wa
chumba chake anaondoka nayo.
Mmoja wa wasaidizi wa karibu wa Jide (jina tunalo) alithibitisha msanii
huyo kuishi hotelini hapo ingawa alikataa kuzungumza lolote kuhusu ndoa
hiyo, kwa kile alichodai kuwa haieleweki.“Ni kweli Anaconda (Jide)
anaishi pale, wewe nenda tu mapokezi kaulize utaelezwa kama hivi sasa
yupo au hayupo,” alisema mtu huyo.
Juhudi za kutafuta ukweli wa sakata la nyota hao zinaendelea huku
ikielezwa kuwa, Gardner ndiye anayetakiwa kutoa tamko kwani ndiye
anayepatika kirahisi katika simu yake ya mkononi.
Imeandikwa na Shakoor Jongo, Gladness Mallya na Chande Abdallah
Alhamisi, 21 Agosti 2014
MAJANGA:JIDE ADAIWA KUHAMIA HOTELINI
07:57
No comments
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)






0 comments:
Chapisha Maoni