Pamoja na watu wengi kumuona Elizabeth Michael aka Lulu kama mtu anayeota ndoto za mchana kutokana na imani yake kuwa siku moja anaweza kuwa Mrs Justin Bieber, ameamua kutoa ufafanuzi na kusisitiza kuwa yupo ‘serious’ na hatokataa tamaa.
“Haya ni hivi wale wa kuandika ndoto za nini cjui…Mara cjui huwezi kumpata na cjui kimepanda kimeshuka…msinijazie comment acha niwape ufafanuzi kdgo,” ameandika muigizaji huyo kwenye Instagram.
“Hivi huyu bwana swala ya yeye kupenda….nimemwachia awapende kina @selenagomez na wengine wote anaotaka kuwapenda…ila swala la yeye kupendwa aniachie mimi….yan hiyo kazi yangu….!!!Sasa Kama ni ndoto Wallah ctaki kuamka,Kama ni ufala…yani ninaukubali kwa asilimia 150%,na mengine mengine yote…sasa Kama nakuchefua,Nina uhakika Zile ndimu za @diamondplatnumz haziwezi kukutosha mana hiki kichefuchefu co cha kuisha,bora utafute mbegu ya Malimao au mbilimbi upande kwako kbsa….Na hili Zoezi ni endelevu…yani kila Jumatatu…Kama Mshahara vile.”
Unahisi kuna uwezekano ndoto za Lulu kumpata Bieber zinaweza kutimia siku moja?
Jumatatu, 18 Agosti 2014
Hutaamini alichoandika Lulu kuhusu kumpata Justin Bieber
06:23
No comments
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni