Staa wa wimbo wa Nakomaa na Jiji, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa na mpenzi wake Nuhu Mziwanda.
STAA wa wimbo wa Nakomaa na Jiji, Zuwena Mohamed
‘Shilole’ amesema sababu kubwa ya yeye kurudiana na mpenzi wake
waliyegombana, Nuhu Mziwanda ni kuombwa msamaha.
Shilole alisema mpenzi wake huyo aligundua kwamba aliteswa na wivu na
kusababisha wagombane hivyo alipotambua kosa lake, aliomba msamaha
wakarudiana na mambo yakawa shwari.
Zuwena Mohamed ‘Shilole’
“Kikubwa ni kwamba ameomba msamaha ndiyo maana na mimi sikuwa na
hiyana, nikapatana naye siku chache tu baada ya kugombana,” alisema
Shilole.Hivi karibuni wawili hao waliripotiwa kuwa wamegombana na kila
mtu kuchukua hamsini zake.