Baada ya jana kushuhudia kalamu ya magoli kwenye mechi ya kwanza ya
nusu fainali ya kombe la dunia kati ya Brazil na Ujerumani, leo hii
imepigwa nisu fainali ya pili kati ya Argentina na Uholanzi.
Matokeo ya mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Sao Paolo ni ushindi uliotokana na mikwaju ya penati wa 4-2 kwa Argentina.
Mechi hiyo ilikuwa ya kukamiana na kucheza kwa kujihami kwa timu zote
mbili iliisha kwa sare tasa katika dakika 120 na hivyo ikaamuriwa
ipigwe mikwaju ya penati.
Waliopata penati kwa Argentina ni Messi, Aguero, Garay, na Rodriguez
wakati Robben na Dirk Kuyt wakifunga penati mbili za uholanzi huku Vlaar
na Sneijder wakikosa.
Argentina sasa itaenda kucheza na Ujerumani fainali jumapili hii,
wakati Uholanzi wakikutana na Brazil jumamosi kugombea medalinya mshindi
wa 3.
Jumatano, 9 Julai 2014
Kilichojiri kwenye mechi ya Uholanzi vs Argentina
17:37
No comments
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni