.

Jumapili, 1 Juni 2014

Matokeo ya Tanzania vs Zimbabwe na Wafungaji Magoli – Ingia Hapa



Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imefanikiwa kuvuka hatua ya kwanza ya michuano ya kuwania kucheza michuano ya kombe la mataifa huru ya Afrika linalotarajiwa kufanyika mwakani.
Stars leo ilikuwa inacheza Zimbwabwe kwenye mchezo wa marudiano baada ya kuwafunga Zimbwabwe 1- 0 uwanja wa taifa wiki moja iliyopita, kwenye mchezo huo Stars imefanikiwa kufuzu baada ya kulazimisha sare ya 2-2.
Zimbwabwe walianza kufunga dakika ya 24, kabla ya Stars kusawazisha dakika kadhaa baadae kupitia Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dakika ya 28.
Muda mchache baadae Thomas Ulimwengu aliongezea Tanzania bao la pili dakika ya 46, kabla ya dakika 10 baadae Zimbwabwe kusawazisha na kufanya matokeo 2-2.
Mpaka refa anapuliza kipenga cha mwisho matokeo yalibaki 2-2, na sasa Tanzania wanaingia hatua ya pili ambapo watacheza na Msumbiji.

0 comments:

Chapisha Maoni