Mtuhumiwa huyo,
William Sebastian (21), mkazi wa Kijiji cha Mlezi alisomewa mashtaka hayo mbele
ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya hiyo, Faustine Kishenyi.
Mwendesha Mashitaka wa
Polisi, Inspekta Samwel Onyango aliieleza mahakama hiyo kuwa mshitakiwa huyo
alitenda kosa hilo Juni 4 mwaka huu saa 9 alasiri huko Mlezi, Ukerewe.
Katika hati ya
mashitaka imeelezwa kuwa mshitakiwa huyo alikutwa akitenda kosa hilo katika
banda la mbuzi nyumbani kwao na mmoja wa wanafamilia.
Katika maelezo hayo,
Onyango alisema mwanafamilia huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu katika
Shule ya Msingi Mlezi, baada ya kushuhudia tukio hilo alikwenda kutoa taarifa
kwa baba yao, Maxmilian Stephan aliyefika na kumkuta mtuhumiwa akiendelea
`kuhangaika’ na mbuzi huyo.
Akifafanua, alisema
kosa hilo ni kinyume cha sheria ya makosa la kujamiiana kifungu namba K/F 154
(1) na (2) C sura ya 16 ya marekebisho ya sheria ya mwaka 2002. Mtuhumiwa
amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande kwa kukosa wadhamini.
0 comments:
Chapisha Maoni