.

Alhamisi, 5 Juni 2014

HUYU NDO BILIONEA MTANZANIA WA KWANZA KUMILIKI GARI LA AJABU HAPA BONGO ONA HAPA




Gari la aina ya Lamboghirn gharama yake kwa hela za Tanzania ni Shillingi Billioni Moja na Nusu. Davis anakuwa Mtanzania wa kwanza kumiliki gari hili la kifahari ambalo ili ulinunue ni lazima uende kiwandani na kutoa order maalum tu na sio vinginevyo. Hata huko USA Star Mweusi wa kwanza na wa mwisho kulimiliki alikuwa ni Mike Tsyon miaka kama 15 iliyopita, lakini vinginevyo wengine wote wamekuwa wakiendesha kwa kukodi tu kutoka kiwandani na sio kulimiliki, Mwaka 1992 Mike Tyson alilinunua kwa USD $ 400,000. Davis ambaye ameoa na ana watoto watatu ni mmoja wa mfano mkubwa sana wa kuigwa kwa wengine kwamba kazi ngumu na nidhamu pamoja na uvumilivu mwisho hulipa na kwamba hakuna njia ya mkato kwenye maisha, na ikipatikana kwa mkato itaishia kwa mkato huo huo, pia Davis amewahi kuwa Mwenyekiti wa Yanga kwa muda mrefu sana na kuipatia mafanikio makubwa sana

0 comments:

Chapisha Maoni