Ajifungua mtoto mwenye kichwa cha nyani Tukio la aina yake na lakushangaza limetokea huko nchini Nigeria baada ya Mwanamke mmoja mkazi wa Kaduna,ambaye jina lake halikuweza kutambuliwa mara moja ameripotiwa kujifungua mtoto anayefanana na nyani kwa sura, masikio na macho.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini Nigeria, tabibu aliyemhudumia mwanamke huyo katika hospitali ya serikali amesimulia tukio hilo lilivyokuwa.
“Alikuja mwanamke mjamzito majira ya saa moja na nusu asubuhi, Jumapili na tukamkimbiza chumba cha wazazi.” Amesema wakati wanamhudumia waliona dalili za kujifungua lakini hazikuwa za kawaida.
“Alikuwa akitokwa damu mfululizo, nikaagiza aje daktari wa wanawake ambaye alimpeleka chumba cha upasuaji kwa lengo la kumfanyia upasuaji. Wakati tunajiandaa, mtoto akaanza alianza akitanguliza miguu. Kwa hiyo daktari akaniambia tuache ajifungue mwenyewe.”
Amesimulia kuwa waliendelea kuyashuhudia maajabu hayo na mwisho wakabaki midomo wazi pale walipomuona mtoto akiwa nusu binadamu nusu nyani na kwamba alifariki muda mfupi baadae.
Amesema mtoto huyo alizaliwa akiwa na uzito wa kilo nne na kwamba mama yake anaendelea na matibabu kwa kuwa alitokwa damu nyingi sana wakati anajifungua.
0 comments:
Chapisha Maoni