.

Jumapili, 1 Juni 2014

AFYA:MADHARA YA UVAAJI WA SURUALI NA NGUO ZA NDANI ZINAZO BANA



Dk alisema siyo tu kuhusu suruali za kubana, lakini nguo zozote za kubana siyo nzuri kuwa mavazi ya kila siku. 
Alieleza kuwa mwili unahitaji kupumua, hali ambayo hufanyika kupitia kutoka jasho kwenye vinyweleo kwenye ngozi na jasho linatakiwa kukauka lenyewe taratibu.
Dk   alisema ikiwa mtu amevaa jinzi ya kubana au nguo ya ndani ya kubana, jasho litagandana kwenye vinyweleo vya ngozi na wakati mwingine inaweza kusababisha
magonjwa ya ngozi kama vile ‘fangasi’, maumivu ya mwili na vipele katika mapaja na sehemu zingine za siri.

“Wanaume ambao wanavaa suruali za kubana wana hatari ya kupunguza kiwango cha mbegu za uzazi.

Na wakati mwingine zinaweza kupungua kwa kiwango kikubwa na kumfanya mwanamume ashindwe kumpa ujauzito mwanamke,” alisema Dk Kafuuza.

Dk   alisema suruali za kubana zina kawaida ya kusukuma ndani sehemu zinazotunza mbegu za uzazi za mwanamume, hali inayosababisha matatizo kama vile uvimbe na ngozi kubabuka.

Nguo za ndani za kubana zinazuia kukuwa kwa mbegu za uzazi.

Wakati joto la kawaida la mwili ni sentigredi 37, mfuko wa mbegu za uzazi wa mwanamume unahitaji kiwango cha joto kati ya sentigredi 35.5 na 36 ili kufanya kazi katika hali ya kawaida.

Dk Charles Kiggundu ambaye ni Mshauri wa Hospitali ya Mulago na Chuo Kikuu cha Afya cha Makerere, alisema joto la mbegu za uzazi za mwanamume linaweza kuongezeka ikiwa mfuko unaozishika utafifia ndani ya mwili kwa muda mrefu, kwa mfano kama mwanamume amevaa nguo ya ndani ya kubana.

Kwa mujibu wa Dk Lawrence Kazibwe wa Hospitali ya Mulago, alisema mbegu za uzazi za mwanamume ziko kwenye mfuko maalumu kwa sababu zinahitaji kuwa zimepoa zaidi ya maeneo mengine ya mwili, ili ziwe kwenye mazingira tulivu.

Alisema lengo hilo linaweza kuvurugika iwapo mwanamume atavaa suruali ya kubana ambayo itazifanya mbegu za uzazi zikose mawasiliano ya kawaida na sehemu nyingine ya mwili, ambayo ni kupata joto linalotakiwa.

“Baadhi ya wanaume wanafikiri kusafirisha mbegu za uzazi pekee kwa mwanamke ndiko kunawezesha mwanamke kupata ujauzito, lakini urutubishaji hauwezi kutokea katika sehemu za kikeni,

kwa kuwa mbegu za uzazi lazima zipite kwenye mrija unaotakiwa kukutana na mayai mengine.


Hivyo basi mbegu za uzazi zinahitaji kuwa na nguvu na nyingi ili ziweze kuyafikia mayai ya kikeni na kuwezesha kupata ujauzito,” alifafanua Kiggundu.

Kiggundu alisema; “Hebu fikiria katika hali ambayo mbegu za uzazi ni chache na dhaifu! Hii ina maana hazitaweza kurutubisha mayai ya kike.

Hivyo unaweza kutoa mbegu za uzazi wakati wa tendo la ndoa, lakini hakuna ubebaji mimba utakaofanyika.”

Mbegu za uzazi ambazo ni dhaifu, kama vile zile ambazo hazina mkia, zenye mkia mkubwa, zenye mkia mdogo, zilizopinda kichwani na zile zenye mikia miwili, haziwezi kupenye kwenye mrija wa kwenda kwenye mayai ya uzazi ya kike.

0 comments:

Chapisha Maoni