.

Jumatano, 28 Mei 2014

‘Zena na Betina’ ya Nisha kutoka Juni 12 badala ya kesho kutokana na msiba wa Rachel







Msanii wa filamu, Salma Jabu aka Nisha ameahirisha kutoa filamu yake ya ‘Zena na Betina’ hapo kesho kutokana msiba wa msanii mwenzao Rachel Haule.



Kupitia Instagram, Nisha ameandika: Habari mashabiki zangu, nyumbani kwetu akifa baba au dada au mwanafamilia yoyote, basi kama kuna aliyetaka kuolewa harusi inaghairishwa, maisha yangu ni filamu, na filamu ni nyumba yangu ya pili, sisi kama Nisha’s film production na Steps Intertainment tumeamua kughairisha kuitoa filamu yetu mliokuwa mkiisubiri kwa hamu ‘Zena na Betina’ ilikuwa itoke tar .29/05/2014 sasa basi tutaisogeza mbele hadi tar.12/06/14 kwa ajili ya kuomboleza misiba hii, samahani kwa usumbufu uliojitokeza, munisamehe sana,tumeguswa sana,kwangu mimi kama Nisha kutoa filamu ni furaha,siwezi kufurahi siku tunayomzika msanii mwenzetu kipenzi Rachel yaani kesho ambayo ndio ilikuwa siku ya kutoka Zena na Betina, nina imani kubwa kama ingekuwa mimi filamu isingetoka kesho na hii ni zawadi yenu Rachel na Adam kuambiana, naomba mnisamehe sana mashabiki zangu,ila nimetazama utu kwanza halafu pesa baadaye.

0 comments:

Chapisha Maoni