KAMPUNI ya Mawasilino ya Vodacom Tanzania, imezindua huduma mpya
ijulikanayo kama ‘Zogo’ ambayo itawawezesha wateja wa mtandao huo kupiga simu
ndani na nje ya mtandao kwa gharama nafuu.

Akizungumza juu ya uzinduzi wa huduma hiyo, Mkuu wa Idara ya
Masoko na Mawasiliano Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa amebainisha kuwa ofa ya
Zogo ni maalum kwa wateja wa Vodacom ambapo sasa tutawawezesha kujipatia muda
mwingi wa maongezi kupitia mtandao
wetu na kwa gharama nafuu zaidi.
wetu na kwa gharama nafuu zaidi.
“Vodacom ni kampuni inayoendeshwa kutokana na mahitaji ya wateja
wake na Zogo imekuja muda muafaka ambapo wateja wetu wameomba muda zaidi wa
maongezi kupitia vifurushi vyetu vya ChekaBombastiki ambavyo vinajumuisha muda
wa maongezi, ujumbe
mfupi na intaneti viongezwe zaidi.”
mfupi na intaneti viongezwe zaidi.”
Twissa aliendelea na kuwatoa hofu wateja wake kuwa, vifurushi
vya ChekaBombastiki vitaendelea kuwepo kama vilivyo kwa wateja wote
wanaopendelea kufuruhia huduma mchanganyiko za dakika za muda wa maongezi,
kutuma ujumbe mfupi, huduma za intaneti
pamoja na kupiga simu kwenda mitandao yote nchini.
pamoja na kupiga simu kwenda mitandao yote nchini.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye uzinduzi wa huduma mpya ya’Zogo’ ambayo itawawezesha wateja wa mtandao wa Vodacom kupiga simu ndani na nje ya mtandao na kujipatia vifurushi kwa gharama nafuu.Ili kujiunga mteja anatakiwa kupiga *149*01#.
“Ofa ya huduma ya Zogo inapatikana kwa wateja wa ndani ya
mtandao wa Vodacom na inaunafuu mkubwa zaidi ukilinganisha na vifurushi vya
ChekaBombastiki. Ofa hii inampatia mteja dakika 30 za muda wa maongezi kwa Sh.
495 tu ndani ya masaa 24, wakati Sh. 645 na 995 zinawapatia wateja dakika 45 na
90 za muda wa maongezi kila moja”alisema Twissa.
Twissa amemalizia kwa kusema kuwa vifurushi vya Zogo
vinapatikana kwa wateja wote wa Vodacom wa malipo ya kabla na baada waliopo
nchi nzima. Ili kupata na kufaidi huduma hiyo wateja wanatakiwa kupiga *149*01#
na kisha kuchagua Zogo, halafu vifurushi
wanavyovipenda zaidi na kufurahia siku nzima.
wanavyovipenda zaidi na kufurahia siku nzima.
Ofa hii imekuja ikiwa hazijapita siku chache tangu kampuni ya
Vodacom ifanye mapinduzi kwa kuzindua huduma nyingine nafuu ya matumizi ya
intaneti ya ‘Uhuru wa Kweli’ kwa wateja wake wote. Huduma hiyo inawapatia fursa
wateja kufurahia huduma za
intaneti kulingana na matumizi yao ya siku, wiki ama mwezi.
intaneti kulingana na matumizi yao ya siku, wiki ama mwezi.
0 comments:
Chapisha Maoni