Watu wa Dar es Salaam
wanasema uzee mwisho Chalinze, Dar es Salaam kila mtu baby, kauli hiyo ilitimia
usiku wa kuamkia Jumanne iliyopita baada ya mmiliki wa Gesti ya GLP ya Mabibo Mwisho
jijini Dar es Salaam, Amos Makelle kunaswa kitandani usiku wa manane na
mfanyakazi wake aitwae Tina.
Bosi huyo na
mfanyakazi wake walinaswa na mchumba wa Tina aitwae Salum Mbonde ambaye
alipenyezewa umbeya huyo na mteja mmoja aliyekodi chumba kwenye gesti hiyo kwa
ajili ya kufuatilia nyendo za wawili hao.
Baada ya mchumba wa
Tina kupewa umbeya huo kuwa wawili hao walikuwa katika harakati za kuchepuka
aliwawekea mtego wa kuwanasa
Waandishi na mchumba wa Tina wakiwa wamelizingira eneo la gesti hiyo mishale ya Saa 8:17 usiku kukiwa kumetulia tuliii... mtonyaji aliyekodi chumba kwa ajili ya kazi maalum aliwatumia ujumbe kuwa mzee Makelle aliyekuwa kwenye chumba chake alitoa shingo kama mara tatu na kuangalia kulia na kushoto kama kulikuwa na mtu aliyemuona.
Ilipotimu saa 8:31, Mzee Makelle akiwa tumbo wazi na kipensi chake aliangalia tena kama hakukuwa na noma, akachomoka chumbani kwake fastafasta kwa hatua za minyato na kuzama chumba namba 104 alimokuwa Tina.
Baada ya dakika chache
waandishi na mchumba wa Tina walizama kwenye chumba hicho na kuwakuta
wawili hao wakiwa kitandani huku Tina akiwa na nguo za ndani.
Walipohojiwa
Tina alikuwa akilia na kumuomba radhi mchumba wake na kusema bosi wake huyo
ndiye alimshawishi kuchepuka naye aliona kitendo cha kumnyima kingesababisha
apoteze ajira yake ambayo anaitegemea.
Mzee Makelle
alipohojiwa, katika hali ya kustaajabisha baada ya kujitetea alianza kumchongea
Tina kwa mchumbaake akidai si mwaminifu.
“Wewe kama huyu ni
mchumba wako hilo mimi nilikuwa silijui, lakini huyu mwanamke juzi tu kalala na
mwanaume mwingine palepale gesti na kama unabisha twendeni nikawaoneshwe kitabu
cha wageni muone jina lake na la huyo bwana,” alisema mzee huyo.
Waungwana waliokuwa
wakimsikiliza mzee Makelle walimtafadhalisha kutozungumza maneno ya kichochezi
na kumtaka ajitete mwenyewe.
Baada ya sakata hilo
kijana huyo alimchukua mchumba wake na kuondoka naye ambapo uchunguzi
umebaini kuwa bado msichana huyo anaendelea kufanya kazi kwenye gesti hiyo.
0 comments:
Chapisha Maoni