Cristiano Ronaldo akishangia kombe na wenzake
Klabu ya Real Madrid iliyo chini ya kocha Carlo Ancelotti jana imenyakuwa ubingwa wa Uefa Champions League 2014 baada ya miaka 12 kwa kuilaza timu ya Atletico Madrid mabao manne kwa moja.
Mpira ulianza kwa timu zote kushambuliana na kucheza kwa kasi hali iliyopelekea
Atletico Madrid kujipatia goli la kwanza kupitia Diego Godin katika kipindi cha
kwanza dakika ya 36.Goli hiyo lilidumu dakika 90 za mchezo mpaka ambapo Real
Madrid walianza kuamka katika dakika 5 za nyongeza baada ya beki wao Ramos
kuisawazishia timu yake katika dakika ya 93, hali ambayo ulifanya mchezo huo
kumalizika kwa 1/1 , matokeo yaliyosababisha kuongezwa dakika 30.
Katika kipindi cha dakika 30 za nyongeza Real Madrid walicheza
kwa nguvu hali iliyolekea timu hiyo kujipatia magoli matatu yaliyofungwa na
Bale, Marcelo na Cristiano Ronaldo kupitia mkwaju wa penati,Ushindi ambao
umewafanya wachukue ubingwa huo.
0 comments:
Chapisha Maoni