.

Jumamosi, 17 Mei 2014

NECTA YABADILISHA VIWANGO VYA UFAULU FORM 6, DIV 1 MWISHO POUNT 7. SOMA ZAID HAPA...!!!


NECTA imetoa mwongozo wa matumizi ya viwango vya Ufaulu (Aprili 2014) ambao umesambwazwa katika shule zote ze sekondari kupitia kwa Maafisa Elimu wa Mikoa. Kwa mujibu wa mwongozo huo Madaraja ya ufaulu kwa Kidato cha Sita 2014 yatapangwa kwa kutumia mfumo uliooneshwa kwenye ukurasa wa 8 wa mwongozo huo ambao ni:
Div I pointi 3-7
Div II pointi 8-9
Div III Pointi 10-13
Div IV awe na D mbili au C moja
Div 0 aliyepata chini ya D mbili.

Kwa mujibu wa mwongozo huo masomo yatakayohesabika kwenye kupanga pointi ni yale tu yaliyoko kwenye tahasusi yaani combination. Kwa maneno mengine suala la kupata cheti kwa mgongo wa Bible Knowledge au Islamic Knowledge litakuwa halipo tena.

0 comments:

Chapisha Maoni